Neno Kutoka kwa baba Askofu

Napenda kuchukua nafasi hii kuwaalika kwa furaha katika tovuti yetu rasmi ya Dayosisi ya Konde, ambapo mtapata fursa ya kujifunza kwa kina kuhusu namna Dayosisi yetu inavyoendelea katika nyanja mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kiroho, elimu, afya, na huduma nyinginezo. KKKT Dayosisi ya Konde imejizatiti katika kuhubiri habari njema za wokovu kupitia YESU KRISTO, na tunajivunia kutekeleza kazi hii kwa ufanisi mkubwa.

Tunayo njozi yenye nguvu inayosema: Ushirika wa Kikristo unaotangaza Habari Njema na Kukuza maisha bora kwa watu wote bila ubaguzi wa aina yoyote. 

Kauli mbiu yetu inasema: ‘Uinjilishaji, uchaji, na ushuhuda mwema.’ Huu ni mwongozo wetu katika huduma zetu, tukiwa na lengo la kuwafikia watu wote kwa upendo na kuwapa matumaini ya maisha bora.

Karibuni sana katika tovuti yetu ili muweze kufahamu kwa undani zaidi kuhusu shughuli na mipango ya Dayosisi yetu. Mungu awabariki sana, na awape neema katika kila jambo linalohusiana na huduma ya Kristo.